You are currently viewing Zingatia haya unapofanya promotion (tangazo la kulipia)

Zingatia haya unapofanya promotion (tangazo la kulipia)

Wengi tunafanya promotion ila hatujui misingi au vitu unapaswa kuzingatia upoanza kurusha tangazo.

Hapo nakuoa baadhi ya vitu vichache tu vya kuzingatia.

1️⃣ Call to Action (C.T.A)
Hii ni sehem unapaswa kuzingatia zaidi maana ndio inashika maamuzi ya mteja wako. Yaani hapa ni sehem unamwambia mteja wako afanye nini baada ya kuwa ameona tangazo lako.

Mf: Apige simu, Atume meseji, aende kwenye profile. Nk

2️⃣ Audience
Hapa unasema sasa unamrenga nani yaani hilo tangazo likawafikie watu gani kwa kuzingatia eneo wanalopatiaka, Umri wao, jinsia zao, vitu wanavyopendelea wakiwa mtandaoni. Nk

Hapa ndipo unaweka bet yako ukikosea kubet umeliwa. 😅

3️⃣ Bajet ya tangazo
Hapa utapanga ulipia kiasi gani kwenye hiyo promotion ili kufikia idadi ya watu unaowataka.

Kumbuka unavyoweke bajet kubwa ndio tangazo linafikia idadi kubwa ya watu.

4️⃣ Tangazo lenye mvuto.
Hakikisha tangazo lako lina mvuto na andiko lene kushawishi mtu kufanya maamuzi.

Hizo tu ni baadhi ya vitu vya msingi sana kuviangalia unapofanya tangazo lako sponsored.

Je post hii imekusaidia?

COMMENT, SHARE, LIKE NA TAG WATU 2

Kama unapenda kupata ushauri na usimamizi wa biashara zako mtandanoni njoo Dm au WhatsApp 0622 578 977.

Cc.
Mr. Niko
@biasharadigitali

Mr Niko

Best digital marketer

Leave a Reply